Bad Advertisement?

News / Reviews:
  • World News
  • Movie Reviews
  • Book Search

    Are you a Christian?

    Online Store:
  • Visit Our eBay Store



  • SWAHILI BIBLIA - 1THESSALONIANS 5

    JANA SURA - IJAYO SURA - AMARA


    5:1 Ndugu, hakuna haja ya kuwaandikieni juu ya nyakati na majira yatakapotukia mambo haya.

    5:2 Maana ninyi wenyewe mwajua kwamba Siku ya Bwana itakuja kama mwizi ajavyo usiku.

    5:3 Watu watakapokuwa wanasema: "Kila kitu ni shwari na salama" ndipo uharibifu utakapowaangukia ghafla! Mambo hayo yatatukia ghafla kama uchungu wa uzazi unavyomjia mama anayejifungua, wala watu hawataweza kuepukana nayo.

    5:4 Lakini ninyi ndugu, hamko gizani, na siku hiyo haipaswi kuwajieni ghafla kama vile mwizi.

    5:5 Ninyi nyote ni watu mnaoishi katika mwanga, watu wa mchana. Sisi si watu wa usiku, wala wa giza.

    5:6 Basi, tusilale usingizi kama wengine; tunapaswa kukesha na kuwa na kiasi.

    5:7 Wanaolala hulala usiku, na walevi hulewa usiku.

    5:8 Lakini sisi ni watu wa mchana na tunapaswa kuwa na kiasi. Tunapaswa kuvaa imani na upendo kama vazi la kujikinga kifuani, na tumaini letu la wokovu kama kofia ya chuma.

    5:9 Maana Mungu hakututeua ili tuangamizwe na ghadhabu yake, bali tuupate wokovu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo,

    5:10 ambaye alikufa kwa ajili yetu, ili tuishi pamoja naye, iwe tu hai au tumekufa.

    5:11 Kwa hiyo farijianeni na kusaidiana ninyi kwa ninyi kama mnavyofanya sasa.

    5:12 Ndugu, tunawaombeni muwastahi wale wanaofanya kazi kati yenu, wale wanaowaongoza na kuwafundisheni kuhusu maisha ya Kikristo.

    5:13 Wapeni heshima kubwa na kuwapenda kwa sababu ya kazi wanayofanya. Muwe na amani kati yenu.

    5:14 Ndugu, tunawahimizeni muwaonye watu walio wavivu, muwatie moyo watu wanyonge, muwasaidie watu dhaifu, muwe na subira kwa wote.

    5:15 Angalieni mtu yeyote asimlipe mwingine maovu kwa maovu, ila nia yenu iwe kutendeana mema daima na kuwatendea mema watu wote.

    5:16 Furahini daima,

    5:17 salini kila wakati

    5:18 na muwe na shukrani katika kila hali. Hayo ndiyo anayotaka Mungu kwenu katika kuungana kwenu na Kristo Yesu.

    5:19 Msimpinge Roho Mtakatifu;

    5:20 msidharau unabii.

    5:21 Pimeni kila kitu: zingatieni kilicho chema,

    5:22 na epukeni kila aina ya uovu.

    5:23 Mungu anayetupatia amani awafanye ninyi watakatifu kwa kila namna na kuzilinda nafsi zenu--roho, mioyo na miili yenu--mbali na hatia yoyote wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.

    5:24 Yeye anayewaita ninyi atafanya hivyo kwani ni mwaminifu.

    5:25 Ndugu, tuombeeni na sisi pia.

    5:26 Wasalimuni ndugu wote kwa ishara ya upendo.

    5:27 Nawahimizeni kwa jina la Bwana muwasomee ndugu zetu wote barua hii.

    5:28 Tunawatakieni neema ya Bwana wetu Yesu Kristo.

    IJAYO SURA - BIBLIA MWELEZO & UTAFUTAJI

    God Rules.NET
    Search 100+ volumes of books at one time. Swahili Biblia Search Engine. Hausa Biblia Search Engine. Afrikaan Bible Search Engine