17:1 Kisha, Yesu akawaambia wanafunzi wake, "Haiwezekani kabisa kusitokee vikwazo vinavyosababisha dhambi; lakini ole wake mtu yule atakayevisababisha.
17:2 Ingekuwa afadhali kwake kufungiwa shingoni jiwe kubwa la kusagia na kutoswa baharini, kuliko kumkwaza mmoja wa wadogo hawa.
17:3 Jihadharini! Kama ndugu yako akikukosea, mwonye; akitubu, msamehe.
17:4 Na kama akikukosea mara saba kwa siku, na kila mara akarudi kwako akisema `Nimetubu`, lazima umsamehe."
17:6 Naye Bwana akajibu, "Kama imani yenu ingekuwa ndogo hata kama chembe ndogo ya haradali, mngeweza kuuambia mti huu wa mkuyu: `Ng`oka ukajipandikize baharini`, nao ungewatii.
17:7 "Tuseme mmoja wenu ana mtumishi ambaye analima shambani au anachunga kondoo. Je, anaporudi kutoka shambani, atamwambia: `Haraka, njoo ule chakula?`
17:8 La! Atamwambia: `Nitayarishie chakula, ujifunge tayari kunitumikia mpaka nitakapomaliza kula na kunywa, ndipo nawe ule na unywe.`
17:9 Je utamshukuru huyo mtumishi kwa sababu ametimiza aliyoamriwa?
17:10 Hali kadhalika na ninyi mkisha fanya yote mliyoamriwa, semeni: `Sisi ni watumishi tusio na faida, tumetimiza tu yale tuliyotakiwa kufanya."`
17:11 Yesu akiwa safarini kwenda Yerusalemu alipitia mipakani mwa Samaria na Galilaya.
17:12 Alipokuwa anaingia katika kijiji kimoja, watu kumi wenye ukoma walikutana naye, wakasimama kwa mbali.
17:15 Mmoja wao alipoona kwamba ameponywa alirudi akimtukuza Mungu kwa sauti kubwa.
17:16 Akajitupa chini mbele ya miguu ya Yesu huku akimshukuru. Huyo alikuwa Msamaria.
17:17 Hapo Yesu akasema, "Je, si watu kumi walitakaswa? Wale tisa wako wapi?
17:18 Hakupatikana mwingine aliyerudi kumtukuza Mungu ila tu huyu mgeni?"
17:19 Halafu akamwambia huyo mtu, "Simama, uende zako; imani yako imekuponya."
17:20 Wakati mmoja, Mafarisayo walimwuliza Yesu, "Ufalme wa Mungu utakuja lini?" Naye akawajibu, "Ufalme wa Mungu hauji kwa namna itakayoweza kuonekana.
17:21 Wala hakuna atakayeweza kusema, `Uko hapa`, au `Uko pale`. Kwa kweli Ufalme wa Mungu uko kati yenu."
17:22 Halafu akawaambia wanafunzi wake, "Siku zinakuja ambapo mtatamani kuona mojawapo ya siku za Mwana wa Mtu, lakini hamtaiona.
17:23 Na watu watawaambieni: `Tazameni yuko hapa`; ninyi msitoke wala msiwafuate.
17:24 Kwa maana kama vile umeme unavyotokea ghafla na kuangaza anga upande mmoja hadi mwingine, ndivyo Mwana wa Mtu atakavyokuwa siku yake.
17:25 Lakini kabla ya hayo, itambidi ateseke sana na kukataliwa na kizazi hiki.
17:26 Kama ilivyokuwa nyakati za Noa, ndivyo itakavyokuwa katika siku za Mwana wa Mtu.
17:27 Watu waliendelea kula na kunywa, kuoa na kuolewa mpaka wakati ule Noa alipoingia katika safina. Gharika ikatokea na kuwaangamiza wote.
17:28 Itakuwa kama ilivyotokea wakati wa Loti. Watu waliendelea kula na kunywa, kununua na kuuza, kupanda mbegu na kujenga.
17:29 Lakini siku ile Loti alipoondoka Sodoma, moto na kiberiti vikanyesha kama mvua kutoka mbinguni na kuwaangamiza wote.
17:30 Ndivyo itakavyokuwa siku ile Mwana wa Mtu atakapofunuliwa.
17:31 "Siku hiyo, yeyote atakayekuwa juu ya paa asishuke nyumbani kuchukua mali yake. Kadhalika, naye atakayekuwa shambani asirudi nyuma.
17:32 Kumbukeni yaliyompata mke wa Loti.
17:33 Yeyote anayetaka kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na yeyote anayeipoteza, ataiokoa.
17:34 Nawaambieni, siku ile usiku watu wawili watakuwa wanalala pamoja, mmoja atachukuliwa na yule mwingine ataachwa.
17:35 Wanawake wawili watakuwa wakisaga nafaka pamoja; mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa."*fc* atachukuliwa na mwingine ataachwa.\ie
17:36 missing
17:37 Hapo wakamwuliza, "Ni wapi Bwana?" Naye akawaambia, "Ulipo mzoga, ndipo tai watakapokusanyikia.